Tangaza Hapa Ad

Mix

‘Ujauzito ni wa Mapacha lakini nikapewa mtoto mmoja Hospitali’ – Asma

on

Siku zimepita tangu sakata la Mwanamke mkazi wa Dar es salaam aitwae Asma kudai kuibiwa mtoto ambaye inadaiwa wakati akifanyiwa Ultra sound alikua na ujauzito wa Watoto mapacha lakini alipokwenda kujifungua aliambiwa amejifungua mtoto mmoja.

Baada ya tukio hilo Serikali ilikaa vikao na wahusika wote kikao kikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Grace Magembe ambapo May 17, 2017 kupitia kwa Msemaji wa Wizara ya Afya, taarifa ilisema Asma Kimwaga alikuwa na mimba ya mtoto mmoja tu.

AyoTV na millardayo.com zimeipata Familia ya Asma Kimwaga na kuongea yafuatayo >>> ‘Naomba viongozi wakubwa Rais Magufuli na Waziri Ummy afatilia swala hili, halikuanzia kwangu kuna wengi tu walitendewa ila hawakuwa na pa kuanzia

Mimi siwezi kutoka na kukukurupuka nikaongopa, nimeshajifungua Temeke hii si chini ya mara mbili sijawahi kuzusha hivyo, nimekwenda na vipimo vyangu na mwenye vipimo kakubali kwenye kikao ila Mganga mkuu tu anawabeba wale

AyoTV na millardayo.com zinaendelea kuutafuta upande wa Mganga Mkuu ili kusikia na upande wake zaidi, kumsikiliza zaidi Asma unaweza kubonyeza play kwenye hii video hapa chini.

VIDEO: ‘Rais Magufuli anakwenda kulishangaza Taifa’ – Mbunge Elibariki Kingu….. bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement