Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Mastaa 10 waliokufa na bado wanaoingiza pesa nyingi…

on

Mtu wangu najua unaweza kushangazwa na hii, mtu aliyekufa kuongoza list ya mastaa wanaingiza pesa nyingi wakati hawapo duniani. Michael Jackson ni mmoja wa mastaa ambao vifo vyao vimechukua headlines tena baada ya Forbes kumtaja kuingiza pesa nyingi zaidi baada ya kifo chake. 

Mfalme wa zamani wa muziki wa Pop, Michael Jackson aliyefariki dunia miaka 7 iliyopita bado ameendelea kuingiza pesa nyingi kiasi cha dola za Marekani milioni 825 mwaka 2016, na kushika nafasi ya kwanza kama star aliyekufa na anayeingiza pesa nyingi zaidi.

Kwa mujibu Forbes, kilichomfanya MJ kuingiza mkwanja mrefu zaidi hata baada ya kifo chake ni baada ya kuamua kuuza hisa zake za sanaa kwenye kampuni ya Sony kwa dola za Marekani milioni 750.

Star huyo wa hit single ya Thriller alinunua hisa za kampuni ya muziki ya Fab Four mwaka 1984 kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 47.5 na kisha kuuza asilimia 50 ya hisa zake kwa kampuni ya Sony mwaka 1995 kwa dola milioni 115.

Mastaa waliotajwa kweny list hiyi ni hawa hapa.

1: Michael Jackson – $825 million

2: Author and cartoonist Charles Schulz – $48 million
3: Golfer Arnold Palmer – $40 million
4: Elvis Presley – $27 million
5: Prince – $25 million
6: Bob Marley -$21 million
7: Theodor ‘Dr. Seuss’ Geisel – $20 million
8: John Lennon – $12 million
9:  Physicist Albert Einstein – $11.5 million
10: Original pin-up girl Bettie Page – $11 million

Tupia Comments

Advertisement