Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Taifa Stars imeanza kwa kipigo maandalizi yake ya AFCON 2019

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars June 13 2019 ilikuwa Alexandria Misri kwa ajili ya kucheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki ikiwa inaelekea kwenye fainali za mataifa ya Afrika 2019, Taifa Stars ilicheza dhidi ya Misri katika uwanja wa Borg el Arab.

Tanzania ikiwa ugenini katika mchezo huo wa kirafiki wamekubali kupoteza kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Ahmed dakika ya 65 ya mchezo huo, licha ya juhudi za washambuliaji wa Taifa Stars wakiongozwa na nahodha wao Mbwana Samatta hawakufanikiwa kusawazisha.

Taifa Stars baada ya kipigo hicho sasa inaaminika itakuwa kocha mkuu Emmanuel Amunike kafanya uchunguzi wa kutosha katika kikosi chake na atakifanyia marekebisho kuelekea kuanza kwa fainali za AFCON 2019, Tanzania imepangwa Kundi C na timu za Senegal, Kenya na Algeria.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments