Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

MAHAKAMANI: Wakili Kibatala ‘ajivua gamba’ kumtetea Wema Sepetu

on

Wakili maarufu Peter Kibatala leo January 10, 2108 amejitoa kumtetea msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, anayekabiliwa na kesi ya dawa za kulevya, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo  wakili Albert Msando ameandika barua ya kuwa wakili mpya wa kumtetea Wema.

Taarifa za mawakili hao, zimetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema amepokea barua ya Kibatala na Msando January 9, 2018.

Hakimu Simba amesema kuwa katika barua hizo, Kibatala ameomba kujitoa kumuwakilisha Wema katika kesi hiyo, huku sababu za kujitoa hazikuwekwa adharani.

Pia Hakimu Simba amesema barua ya Msando ameomba amtetee Wema Sepetu, hivyo anaomba apewe muda wa kupitia jalada la kesi hiyo ili aanze kumuwakilisha mahakamani.

Hakimu Simba amesema anakubaliana na barua za mawakili wote wawili, hivyo anaahirisha kesi hiyo hadi February 8,2018.

Mbali na Wema, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

MAHAKAMANI: Wema Sepetu hakufanyiwa upekuzi kwenye maungo yake

MAHAKAMANI: Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’

 

Soma na hizi

Tupia Comments