Tangaza Hapa Ad

AyoTV

“Utaratibu unafanywa kumpeleka Lowassa Mahakamani” – Tundu Lissu

on

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu leo July 17, 2017 amekutana na Waandishi wa Habari Dar es salaam na kuzungumzia ishu mbalimbali ikiwemo tukio la kukamatwa kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dr. Vincent Mashinji na Edward Lowassa kupelekwa Mahakamani.

Amesema “Muda mfupi uliopita katibu mkuu wetu Dr. Vicent amepata dhamana ya Polisi Bamba bay na tumeambiwa aripoti kesho sasa haieleweki ni kwa RPC, Mkuu wa mkoa au kwa Mkubwa gani mwingine lakini tumeambiwa kwamba anatakiwa aripoti mahali”

Hivi tunavyozungumza utaratibu unafanywa wa kumpeleka Edward Lowassa, Waziri mkuu mstaafu pamoja na Mgombea Urais aliepigiwa kura na zaidi ya Watanzania milioni 6  kufikishwa Mahakamani na kushitakiwa kwa kosa lilelile ambalo alishtakiwa nalo Mwalimu Nyerere miaka 60 iliyopita, kosa la uchochezi

Kutazama kila alichokieleza Tundu Lissu unaweza kubonyeza play hapa chini kwenye hii video kufahamu

ULIPITWA? Lowassa alivyohojiwa Makao makuu ya Polisi? bonyeza play hapa chini kujionea

ULIPITWA? Lowassa atumia dakika 30 kuingia na kutoka Makao Makuu ya Polisi, tazama hapa chini kwenye video

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement