Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Saa 48 alizopewa Rais Jacob Zuma

on

Stori kubwa inayoendelea kushika headlines katika vyombo vya habari Afrika Kusini hasa katika Shirika la Utangazaji la nchi hiyo SABC ni kuhusu President Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu, wadhfa wake huo.

Saa hizo 48 zimetolewa baada ya mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na Chama Tawala cha nchini humo ANC. Chama hicho kilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa Chama ana kwa ana ya kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madarakani.

Lakini haijulikani bado kwamba Rais Zuma alipokeaje ujumbe huo. Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama hicho kumng’oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuwa mrefu na wenye madhara zaidi kwa chama cha ANC.

Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa anaongoza shinikizo la kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye kushika pia nafasi hiyo, ambaye pia ameahidi kupambana na rushwa iliyokithiri na kukijenga upya chama cha ANC, wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mwakani

“SIJAWAHI NA SITAKAA NISHIRIKIANE NA DIWANI NA MBUNGE WA CHADEMA, FULL STOP” RC MNYETI

Soma na hizi

Tupia Comments