Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

‘Kibarua kimeota nyasi’ kwa walimu na maafisa elimu 43 wilayani Kiteto…..kisa?

on

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti ametengua nafasi za wakuu wa shule za msingi zaidi ya 30 pamoja na maafisa elimu kata 13 wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kutokana na kuzembea kazini na kusababisha wilaya kushuka kitaaluma.

Uamuzi huo ameutoa baada ya kupokea taarifa ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Tumaini Magesa kwenye kikao kazi cha kukutana na watendaji wa serikali, na kutoridhishwa na kiwango cha ufaulu, huku akimuonya Afisa Elimu wa shule za msingi na utumishi kushindwa kuwachukulia hatua watumishi.

Shule za wilaya hiyo zimeshindwa kufikia kiwango cha ufaulu wa wastani wa asilimia 50 katika mtihani wa taifa wa darasa la saba kwa mwaka 2017, kitendo kilichomkasirisha Mkuu huyo wa Mkoa.

January hii Mbunge Catherine Ruge Chadema, atawafikia watoto 413.

JPM IKULU: “Lowassa hakuwahi kunitukana hata siku moja”

Soma na hizi

Tupia Comments