Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

AyoTV

“Tusiingize siasa kwenye mambo ya maendeleo” –Dr Tulia (+Video)

on

Naibu Spika Dr Tulia Ackson amefanya ziara katika baadhi ya maeneo Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya ikiwa ni kutekeleza baadhi ya ahadi alizowahi kuzitoa katika kusaidia maendeleo, kwanza alianza kwa kutoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni tano katika shule ya sekondari Bujela huku akiwataka wananchi kuacha kuingiza siasa kwenye mambo ya maendeleo.

Akiwa katika shule ya Bujela Dr Tulia alisema>>>“Ndugu zangu niwasihi jambo moja ambalo hata Rais Magufuli husisitiza, tusiingize siasa kwenye mambo ya maendeleo kwasababu bila hivyo hatutapiga hatua, leo kama TULIA TRUST tuliahidi vifaa vyenye thamani ya Milioni tano na tayari tumetekeleza kwa kuja navyo vikiwemo bati, mbao, mchanga, saruji, chokaa, rangi, vioo, nondo n.k” –Dr Tulia

Full video ya Dr Tulia nimekuwekea hapa chini talari…

Baba Diamond Kafunguka ishu ya Mama Diamond kuolewa “Msiniingilie na mama Diamond”

Soma na hizi

Tupia Comments