Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Stori Muhimu

AUDIO: Sababu za M/Kiti kamati ya Wizara ya Viwanda kujiuzulu leo

on

Leo March 20, 2017 aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya viwanda, biashara na mazingira Dkt. Dalaly Peter Kafumu amemuandikia barua ya kujiuzulu nafasi hiyo ya Uenyekiti Spika wa Bunge Job Ndugai kwa madai kuwa anahitaji muda wa kupumzika na kuwatumikia wananchi wa jimbo lake.

Dalaly Kafumu amekubali kukaa kwenye exclusive interview ya millardayo.com na kuzitaja sababu zote za kufanya maamuzi hayo yeye pamoja na Naibu wake.

Ni kweli nimejiuzulu kwasababu nataka nipate muda mwingi wa kuhudumia jimbo langu, nimejikuta nakuwa bize sana na kamati hivyo kusababisha kushindwa kushiriki vikao vya jimbo‘ –Dalaly Kafumu

Ni kweli amejiuzulu kwa shinikizo baada ya kudaiwa Serikali imeingilia madaraka ya bunge? Kafumu amesema..>>>’Hakuna shinikizo kama hilo bali nimeamua mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kunishinikiza kuendelea au kubaki katika nafasi hiyo‘ –Dalaly Kafumu

Unaweza kuendelea kumsikiliza Dalaly Kafumu hapa chini kwenye hii sauti…

VIDEO: ‘Mimi ni Rais ninayejiamini, siwezi nikapangiwa mtu’-JPM 

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments