Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Mashahidi hawajui rangi ya mkojo wa Masogange…ilichoamua Mahakama?

on

Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elia Mulima leo August 28, 2017 amesema hakumbuki na hafahamu mkojo wa mrembo wa Bongo Agnes Gerald maarufu Masogange una rangi gani.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, Shahidi huyo amesema anamfahamu Masogange baada ya kufikishwa kwenye ofisi za Mkemia, ambapo alimuona majira ya saa 8 mchana na kueleza kuwa alipokea sampo ya mkojo wa Masogange kutoka kwa Detective Copro Sospeter baada ya kumpa maelekezo ya kuchukua sampuli hiyo.

Hata hivyo, Shahidi huyo alipoulizwa na Wakili wa Utetezi, Ruben Semwanzi kama anakumbuka mkojo wa Masogange una rangi gani?

Shahidi huyo alidai kuwa hajui una rangi gani maana kila mtu mkojo wake una rangi tofauti ambapo alisema>>>”Hivyo nilichukua sampuli ya mkojo wake na kuufanyia uchunguzi ambapo nilibaini una chembe chembe za dawa za kulevya Metabolite ambayo ni zao la Heroin.”

Aidha, Shahidi wa pili, ambaye ni Mpelelezi kutoka Ofisi ya ZCO, WP Judith amesema alimchukua Masogange February 15, 2017 hadi kwa Mkemia Mkuu baada ya kupewa maelekezo na Kaimu Mkuu wa Upelelezi, Ramadhan Kingai kwa lengo la kumpeleka kwa Mkemia baada ya kuambiwa Masogange anatuhumiwa kutumia na kusafirisha dawa za kulevya.

>>>”Nikiwa mapokezi kwa Mkemia nilipewa chupa ya plastic namba 446, kisha nikaelekezwa nimpeleke mshtakiwa chooni ili nichukue sampo ya mkojo wake.”

Alidai kuwa aliingia na Masogange hadi chooni na alisimama mlangoni ili kuthibitisha kama Masogange angekojoa kweli ama la na baada ya kuchukua sampuli hiyo alimkabidhi chupa Copro Sospeter ambaye alikuwa na fomu kisha wakaiwasilisha mapokezi.

Hata hivyo, shahidi huyo alipoulizwa na Wakili Semwanzi kuwa mkojo wa Masogange una rangi, alisema hakumbuki rangi akisema>>>”Sikumbuki rangi, isipokuwa inafahamika rangi ya mkojo ni ipi, ila kama ulikuwa wa rangi ya Njano Mpauko.”

Baada ya kutolewa ushahidi huo, kesi imeahirisha hadi August 31, 2017.

ULIPITWA? LISSU MAHAKAMANI TENA: ni kuhusu kesi yake ya ‘Dikteta uchwara’

Soma na hizi

Tupia Comments