PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Top Stories

Mbwa alivyoiokoa familia dhidi ya kuteketea kwa moto

on

Leo June 13, 2018 Nakusogezea stori kumhusu Mbwa anayejulikana kama Sasha ameikoa familia moja mjini California nchini Marekani baada ya kuiamsha familia hiyo alipogundua kuwa nyumba wanayoishi inawaka moto.

Taarifa zinasema kuwa Sasha baada ya kuona nyumba yao inawaka moto aliiamsha familia kisha akaenda katika chumba cha mtoto na kumbeba na kuanza kuondoka naye kumpeleka sehemu salama kwa kung’ata diaper yake.

Kwa mujibu wa Latana Chai ambaye ndiye mmiliki wa mbwa huyo amesema kuwa Sasha aliiamsha familia hiyo kwa kubweka sana na kulazimisha kutaka kuuvunja mlango wa nyuma wa nyumba hiyo kitu ambacho sio kawaida yake.

“Nilifungua mlango na mara Sasha akaingia na kwenda kwenye chumba cha mtoto na kuanza kumbeba kumpeleka sehemu salama kwa kung’ata Diaper” alisema Chai.

Aidha Chai amesema kuwa Mbwa huyo amekuwa na mahusiano mazuri sana na mtoto wake huyo na wanamshukuru kwa kuwa shujaa wao.

Maneno ya Rais Magufuli kwa TB Joshua katika Birthday yake

Soma na hizi

Tupia Comments