Michezo

Didier Deschamps kamuona tena Anthony Martial wa Man United

on

Good News imemdondokea tena mshambuliaji wa Man United Anthony Martial baada ya kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kwa mara ya kwanza toka mwezi March mwaka 2018, Martial alikuwa hajaitwa timu ya taifa ya Ufaransa kwa muda wa zaidi ya miezi 8.

Martial akiwasili kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa.

Martial ambaye amekuwa na kiwango kizuri akiwa na Man United kwa wiki za hivi karibuni, amejumuishwa tena katika kikosi baada ya uwezo wake kumvutia kocha mkuu wa Ufaransa Didier Deschamps, akiwa katika mechi 7 zilizopita na Man United amefanikiwa kufunga magoli 7.

Pogba akiwasili kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikosa michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi baada ya kutoitwa timu ya taifa ila anarudi baada ya kurudisha imani kwa kocha wake Jose Mourinho ambaye anampa nafasi ya kucheza kutokana na kiwango chake kuimarika.

Mbappe akiwasili kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa.

Hata hivyo licha ya kukosa katika mchezo wa Manchester Derby kutokana na kuwa majeruhi, Paul Pogba nae amejumuishwa katika kikosi cha Ufaransa kitakachocheza dhidi ya Uholanzi mchezo wa Nation League November 16 na November 20 wakicheza mchezo dhidi ya Uruguay wa kirafiki.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments