Premier Bet

Michezo

OFFICIAL: Man United imemtangaza mbadala wa muda wa Jose Mourinho

on

Club ya Man United leo imefikia maamuzi ya kumtangaza kocha wao mpya wa muda atakayemrithi kocha Jose Mourinho katika club hiyo, uamuzi huo unatangazwa leo ikiwa ni siku moja imepita toka club ya Man United itangaze kusitisha ajira ya Jose Mourinho ndani ya Old Trafford.

Man United leo imemtangaza mchezaji wao wa zamani raia wa Norway, Ole Gunnar Solskjaer kuwa ndio kocha wao mpya atakayemrithi Jose Mourinho hadi mwisho wa msimu wa 2018/2019 watakapotangaza kocha mpya wa kudumu, Ole Gunnar Solskjaer  atakuwa kocha wa Man United akishirikiana na  Mike Phelan na Michael Carrick na Kieran McKenna.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Ole Gunnar Solskjaer aliyetangazwa kuwa kocha wa muda wa Man United, aliwahi kuwa mchezaji wa zamani wa Man United kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2007 na aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Norway, Solskjaer kabla ya kujiunga na Man United kama kocha wa muda alikuwa akiifundisha Molde na amewahi kuifundisha Cardiff City na timu ya Man United ya wachezaji wa akiba.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments