Michezo

Omar Colley ametangana rasmi na Mbwana Samatta KRC Genk

on

Baada ya headlines za wiki kadhaa kuhusiana na beki wa kimataifa nahodha wa Gambia aliyekuwa anachezea club ya KRC Genk ya Ubelgiji Omar Colley kuripotiwa kuwa ataondoka club hiyo leo amehama rasmi.

Omar Colley ambaye katika kipindi cha miaka miwili akiichezea KRC Genk ya Ubelgiji wakiwa marafiki wa karibu Mbwana Samatta, leo ametangaza rasmi kujiunga na club ya Sampdoria ya Italia.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Omar Colley kabla ya kujiunga na KRC Genk mwaka 2016, alikuwa akiichezea Djurgårdens IF ya Sweden kipindi hicho akicheza na mkenya Michael Olunga ambaye nae kwa sasa anaichezea Girona ya Hispania.

Samatta na Omar Colley walipokuwa Macca Saudi Arabia katika ibada ya umrah

FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018

Soma na hizi

Tupia Comments