Michezo

Pogba kamuonya kocha wake Jose Mourinho

on

Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Club ya Man United ya England Paul Pogba ameamua kumtolea uvivu kocha wake Jose Mourinho na kuwa asimsingizie kama yeye ndio tatizo la timu yake ya Man United kufanya vibaya.

Pogba na Mourinho wanadaiwa kuingia tena katika msuguano baada ya mchezo wa Man United dhidi ya Southampton uliyomalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2, wakiwa ugenini katika uwanja wa St Marry, Mourinho anadaiwa kuwa katika vyumba vya kubadilishia nguo alimlaumu Pogba kupoteza mipira kiholela.

Hivyo staa huyo nae anadaiwa kumjibu kocha wake kuwa asimsingiezie kuwa yeye (Pogba) ndio chanzo cha kufanya timu ishindwe kucheza vizuri, mtandao wa The Sun unaripoti kuwa Pogba amemuonya Mourinho kuwa asimpakazie kuwa yeye ndio kiini cha matatizo ndani ya timu.

Man United leo wanacheza na Arsenal game ya 15 ya Ligi Kuu Ubelgiji katika uwanja wa Old Trafford lakini wanatajwa kuingia na presha kubwa mbele ya mashabiki wao kutokana na kutokuwa na msimu mzuri safari hii ukilinganisha na Arsenal watakaoingia wakiwa na rekodi ya kutopoteza kwa game 19 mfululizo msimu huu za mashindano yote, Man United wapo nafasi ya 8 EPL wakiwa na point 22.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments