Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Huu ndio mtihani wa kwanza wa Unai Emery ndani ya Arsenal

on

Ratiba ya Ligi Kuu England msimu wa 2018/2019 imetoka leo na tayari imetangazwa rasmi kuwa Ligi hiyo itaanza August 11 2018 kwa michezo 10 ya ufunguzi kuchezwa katika viwanja mbalimbali England.

Arsenal ambao wataanza msimu mpya wa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza wakiwa na kocha mpya Unai Emery baada ya kufundishwa na kocha Arsene Wenger kwa miaka 22, wamepangwa kuanza kupambana na Mabingwa watetezi Man City.

Kikosi cha Arsenal kitakuwa nyumbani kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Man City katika uwanja wao wa Emirates, huu unatajwa kuwa ni kama mtihani wa kwanza wa Unai Emery kudhihirisha ubora wake katika kikosi cha Arsenal.

FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018

Soma na hizi

Tupia Comments