Premier Bet

Michezo

Mourinho anaondoka Man United ila atakumbukwa kwa rekodi hii

on

Club ya Man United imetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu mreno Jose Mourinho kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo ambao umekuwa ukienda kwa kusuasua msimu huu, uongozi umeamua kumfuta kazi Jose Mourinho na kumtangaza Michael Carrick ambao ni mchezaji wao wa zamani kuwa kocha wa muda wa timu hiyo.

Jose Mourinho anafutwa kazi ikiwa ni miaka miwili imepita tokea aajiriwe kuwa kocha wa timu hiyo mwaka 2016, moja kati ya tukio kubwa linalochukua headlines kuhusu Jose Mourinho ni kuhusiana na kufanana kidogo tarehe ya leo December 18 2018 kufutwa kazi Man United inataka kufanana na siku ya December 17 2015 aliyofutwa kazi na Chelsea zikiwa zimepishana siku moja.

Hadi sasa Man United wapo nafasi ya 6 katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu, wakicheza michezo 17, sare michezo mitano, ushindi michezo 7 na wamepoteza michezo mitano wakiwa na point 34, hata hivyo Mourinho anaondoka Man United akiwa atakumbukwa kwa rekodi ya kipekee akiwa ni kocha wa kwanza wa Man United katika msimu wake wa kwanza na kutwaa mataji mawili ya UEFA Europa League na Kombe la Ligi.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments