Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

MAHAKAMANI: Kilichosababisha Aveva ashindwe kufika Mahakamani leo

on

Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha wa USD 300,000 ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu ana matatizo ya figo.

Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa TAKUKURU, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi haujakamilika lakini amepewa taarifa kuwa Aveva anaumwa.

Mbali ya Aveva mshtakiwa mwingine katika kesi iyo ni Geofrey Nyange maarufu kama Kaburu.

Swai ameeleza kuwa amepewa taarifa kutoka Magereza kuwa Aveva hakufika mahakamani kwa sababu ana matatizo ya figo.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa alikubaliana na maombi ya kutaka kumuhoji Kaburu, ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi January 25, 2018.

MAHAKAMANI: Kesi ya ‘Ndama mtoto wa Ng’ombe’ nyaraka zinatoka Australia

Mahakama yakwama kutoa hukumu ya ‘Scorpion’

 

Soma na hizi

Tupia Comments