Top Stories

Wafanyabiashara 2 wapandishwa kizimbani kwa kusafirisha madini ya Bil 1.5 bila leseni

on

Mfanyabiashara maarufu nchini Naushad Mohammed Suleiman (63) na Ali Makame (36) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya kusafirisha madini ya dhahabu vipande saba vyenye thamani ya Sh.Bil 1.5 bila leseni.

Wafanyabiashara hao wamesomewa makosa yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na Wakili wa serikali, Jehovanes Zacharia ambaye alidai washtakiwa wanakabiliwa na makosa mawili ikiwemo uhujumu uchumi.

Wakili Zacharia alidai kosa la kwanza la kula njama linawakabili washtakiwa wote ambapo walilitenda katika tarehe tofauti kati ya November mosi na 29, 2017 wakati kosa jingine ikiwa ni la kusafirisha madini bila kibali ambalo walilitenda November 29, 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar.

Baada ya kusomewa mashtaka yao, Hakimu Mashauri alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu kitu chochote kwa sababu kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi na baada ya Wakili Zacharia kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi December 20,2017.

Ulipitwa na hii? MAHAKAMANI: Kesi ya Aveva na Malinzi

Soma na hizi

Tupia Comments