PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Simba inashusha wachezaji wa kimataifa, mwingine ametajwa hapa kimya kimya

on

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya wekundu wa Msimbazi Simba inaonekana kujiandaa vyema kwa ajili ya mashindano mbalimbali kutokana na kuzidi kujiimarisha, Simba ambayo inalenga kuleta ushindani kimataifa inazidi kushusha vifaa.

Kuna habari zimeanza kuripotiwa kuwa club ya Simba SC baada ya kumshusha beki wa zamani wa Azam FC Pascal Wawa na kuanza kufanya mazoezi na timu ili kumuangalia Simba sasa imeshusha mwingine kutoka Gor Mahia ya Kenya Meddie Kagere.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Kagere ambaye inadaiwa amefikia makubaliano na Simba baada ya kufanya mazungumzo na kaimu wa Rais wa club Salim Abdallah, aliifunga Simba SC katika mchezo wa fainali ya SportPesa Super Cup, Simba SC kwa sasa inajiandaa na mashindano ya Kagame Cup yatakayoanza July 28 2018 .

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments