Top Stories

Uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli leo February 19,

on

Stori kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu leo February 19, 2018 ni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa  Mwenyekiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH).

Ambapo Rais Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa imesema uteuzi wa Prof. Maboko unaanza leo February 19, 2018.

Prof. Maboko ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI KWA VYOMBO VYA DOLA KWA WALIOSABABISHA AKWILINA KUPIGWA RISASI

 Soma na hizi

Tupia Comments