Michezo

Kama ulipitwa na Burudani ya Ligi Kuu Tanzania bara

on

Ligi Kuu Tanzania bara iliendelea leo tena kwa game nne kuchezwa katika viwanja mbalimbali wakati Mabingwa watetezi wa Tanzania Simba SC walikuwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga kucheza dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wao wa ugenini.

Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi kwa kuifunga JKT Tanzania kwa magoli 2-0, magoli yote ya Simba SC yakifungwa na Mrwanda Meddie Kagere dakika ya 13 na dakika ya 38, hivyo Simba imeendeleza wimbi la kuonesha kuwa wanatamba popote sio uwanja wa Taifa pekee.

Matokeo hao yanaifanya Simba SC kuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa wamecheza game 11 sawa na Azam FC wanaoongoza Ligi kwa tofauti ya point moja, JKT Tanzania wao wapo nafasi ya saba wakiwa na jumla ya point 18 wakicheza game 12.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments