AyoTV

Wadhamini wa FC Barcelona wameahidi kumpa zawadi hii mchezaji bora Ndondo Cup 2018

on

Michuano ya mchangani maarufu kama Ndondo Cup 2018, Jumatatu ya May 28 katika viwanja vya Escape One droo ya Makundi ya michuano hiyo ilichezeshwa chini ya mwenyekiti wa Ndondo Cup Shaffid Dauda na mchezaji wa Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa Baroka FC ya Afrika Kusini Abdi Banda.

Wakati wa upangaji wa makundi ya michuano ya Ndondo Cup 2018 baada ya hapo mkuu wa mauzo kwa Afrika wa kampuni ya uuzaji wa vifaa vya umeme ya Beko Jason Picken alitangaza zawadi ya mchezaji bora wa michuano hiyo kwa mwaka 2018.

Beko ambao ni moja kati ya wadhamini wa Ndondo Cup 2018 kupitia kwa Jason Picken wametangaza zawadi ya kumpeleka mchezaji bora wa mashindano ya Ndondo Cup katika club ya Besikas ya Uturuki kufanya majaribio ya wiki moja ambapo kampuni hiyo watagharamia kila kitu.

Kama hufahamu club ya Besiktas ni moja kati ya vilabu vikubwa Uturuki na vimewahi kuchezewa na mastaa wakubwa mbalimbali kama Demba Ba raia wa Senegal aliyewahi kuichezea pia na Chelsea ya England, Beko pia ni wadhamini wa club ya Besiktas na FC Barcelona ya Hispania.

Yametimia maneno ya mchambuzi mkongwe Dr Leaky kuhusu Champions League

Soma na hizi

Tupia Comments