Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA: Oliver Giroud amefufua matumaini ya Chelsea kumaliza TOP 4

on

Wakati Mabingwa wa Ligi Kuu England msimu 2017/2018 Man City wakikabidhiwa taji lao la Ubingwa wa EPL leo, Club ya Chelsea ilikuwa mwenyeji wa club ya Liverpool katika uwanja wao wa Stamford Bridge kucheza mchezo wa kuwania nafasi ya nne ya Ligi Kuu England.

Chelsea ambaye yupo nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu wanapambana kuhakikisha wanamaliza msimu wakiwa nafasi nne za juu ili wapate nafasi ya kushiriki michuano ya UEFA Champions League msimu ujao.

Leo wakiwa nyumbani  wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Oliver Giroud dakika ya 32, ushindi ambao umewafanya wawe nafasi ya tano lakini kwa tofauti ya point 2 dhidi ya Tottenham Hotspurs aliyepo nafasi ya nne kwa kuwa na point 71 Chelsea wakiwa na 69.

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa

VIDEO: Emmanuel Okwi hawezi kupata presha kwa rekodi ya Tambwe VPL

Soma na hizi

Tupia Comments