Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

BAD NEWS: Jose Mourinho kuhusu hali ya Lukaku

on

Club ya Manchester United ambayo usiku wa December 30 2017 imelazimishwa sare tasa (0-0) katika mchezo wake wa Ligi Kuu England dhidi ya Southampton, kocha wao Jose Mourinho ametangaza habari mbaya kuhusu safu yake ya ushambuliaji kupungukiwa nguvu.

Jose Mourinho sasa amethibitisha kuwa atawakosa kwa muda mrefu kidogo Romelu Lukaku aliyeumia kwenye game ya leo dhidi ya Southampton na mshambuliaji wake Zlatan Ibrahimovic ambaye yupo majeruhi anasumbuliwa na goti, Mourinho baada ya game aliongelea kuhusu Lukaku.

Lukaku ametolewa nje dakika ya 14 baada ya kuumia kichwani na baada ya game Jose Mourinho aliongea na waandishi wa habari na kusema “Ukiona mchezaji anatolewa kama alivyotoka Lukaku basi ujue anaweza kukaa nje kwa walau mechi hata mbili”

“Nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba”-Haji Manara

Soma na hizi

Tupia Comments