Premier Bet

Michezo

Baada ya kipigo cha 7-1 cha Monaco vs PSG, Monaco wametangaza kulipa fidia

on

Uongozi wa Club ya AS Monaco ya Ufaransa leo umetangaza maamuzi magumu ya kuamua kulipa fidia kwa mashabiki wake waliyosafiri kutoka Monaco hadi Paris kuangalia game ya AS Monaco dhidi ya PSG katika uwanja wa Parc des Princes.

AS Monaco wamefikia maamuzi hayo baada ya timu yao usiku wa jana kuchukua kipigo cha magoli 7-1 dhidi ya PSG, kitu ambacho viongozi wanaamini timu yao haikuwafanyia fair mashabiki waliyosafiri kwenda kutazama game hiyo na ikaisha kwa kipigo cha kidhalilishaji.

Taarifa rasmi ya club hiyo kuhusiana na uamuzi huo imetolewa kupitia ukurasa wao wa twitter na kueleza kuwa wiki hii watatangaza mfumo utakaotumika kuwarudishia fidia mashabiki wao waliohudhuria game yao dhidi ya wenyeji PSG.

ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1

Soma na hizi

Tupia Comments