Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Kim Kardashian ameanza mipango ya kufungua kesi ya kudai Talaka dhidi ya Kanye West

on

Kama ilivyo kawaida, kazi yangu ni kuhakikisha haupitwi na chochote, na leo nimeipata hii kutoka kwa Kim Kardashian ambaye ni mke wa rapa Kanye West anayedaiwa kuanza mipango ya kufungua kesi ya madai ya talaka dhidi ya mume wake huku akitaka mahakama impe haki kamili ya malezi ya watoto wao wawili.

Huenda ikakushangaza hii kwasababu ya kile kinachofahamika kuwa rapa Kanye West hayuko sawa kiafya kwasasa baada ya kulazwa Hospitali siku chache zilizopita kutokana na kudaiwa kuwa na msongo wa wa mawazo pamoja na uchovu mwingi.Kwa mujibu wa mtoa taarifa ambaye inaelezwa kuwa ni rafiki wa karibu wa Kim amesema kuwa pamoja na magumu anayoyapitia rapa huyo, Kim ameamua kuanza mipango ya kudai talaka ikiwa ni siku chache baada ya ripoti ya Daktari kueleza kuwa Kanye West asikae karibu na silaha ya aina yoyote.

Taarifa zilizotolewa na mtandao wa Us Weekly zimeeleza kuwa Kim anakamilisha kesi ya madai ya talaka ambayo itampa haki zote za kulea watoto wao wiwili North mwenye miaka mitatu pamoja na Saint ambaye ametimiza mwaka mmoja Jumatatu ya wiki hii Dec, 5. 2016

“Japokuwa itachukua muda mrefu sana kulitekeleza hilo, lakini Kim hahitaji tena kuendelea na ndoa yake. Na hili linatokea wakati ambao Kim amekuwa msaada mkubwa kwa mume wake ambaye yuko kwenye matatizo ya kiakili kwasasa, lakini bado ameonesha kutotaka watoto wake wakae karibu na Kanye” – Rafiki wa Kim

Mapema wiki hii iliripotiwa kuwa Kim na Kanye watangana kutoka kuishi nyumba moja na sasa kila mmoja anaishi kivyake na hii ni baada tu ya Kanye kuruhusiwa kutoka Hospitali. 

VIDEO: Nimekuwekea hapa list ya wasanii watakaokuwemo kwenye albam mpya ya NavyKenzo. Tazama hapa.

Soma na hizi

Tupia Comments