PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Habari za Mastaa

Show ya Dallas yamvunja mguu Childish Gambino

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapper Childish Gambino amevunjika mguu alipokuwa akitumbuiza kwenye ukumbi wa American Airlines Center  Dallas Marekani Jumapili ya September 23,2018.

Taarifa zinaripoti kuwa rapper huyo alionekana kukosea step wakati akitoa burudani jukwaani na kabla ya kumalizika kwa show, dakika 30 za mwisho wengi walimshuhudia akianguka chini na hali yake kuonekana sio nzuri.

Rappa huyo alishindwa kuendelea kutoa burudani na hivyo kulazimika kuondoka jukwaani na kuwakumbusha mashabiki kuwa hiyo ndio ziara yake ya mwisho ya ‘This is America Tour’ na kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano walioutoa kwake.

Muonekano wa Duka la Wema Sepetu

Soma na hizi

Tupia Comments