Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Yanga nao hao Kenya safari ya kuwania kucheza na Everton

on

Saa kadhaa baada ya watani zao wa jadi Simba SC kuelekea Nairobi Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup wakishirikisha timu 8, Yanga nao jioni ya May 31 wamepanda ndege kuelekea Nairobi na baadae Nakuru yatakapofanyikia mashindano hayo.

Yanga wanaelekea katika mashindano hayo ambapo chachu ya ushindi wa mashindano hayo, inatokana na zawadi kubwa inayotolewa na SportPesa kwa Bingwa wa michuano hiyo kupelekwa Liverpool England kucheza dhidi ya Everton katika uwanja wa Godson Park.

Michuano ya SportPesa Super Cup itaanza June 3 hadi June 10 2018 na Yanga wao wapo Kundi moja na timu za Home Boys, Gor Mahia na JKU ambao ni Mabingwa wa Zanzibar.

VIDEO: Mazoezi binafsi ya Simon Msuva na mdogo wake wakati huu akiwa likizo

Soma na hizi

Tupia Comments