Michezo

Haji Manara baada ya kuenea kwa taarifa za kufungiwa

on

Baada ya taarifa za uongo kusambazwa mitandaoni kuwa afisa habari wa Simba Haji Manara amefungiwa na Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia, leo TFF wametoa taarifa rasmi ya kukanusha taarifa hizo kuwa ni uongo.

Baada ya TFF kukanusha taarifa hizo, afisa habari wa club ya Simba SC Haji Manara alitumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe mzito kuhusiana na wale waliozusha taarifa hizo.

“SHUUUU !!!! Nyumba hujengwa kwa Matofali, Simenti, Mchanga na hata Nondo..haijengwi kwa Hasadi,Choyo Chuki na Roho mbaya…mshanizushia kifo, nipo hai. hili nalo limedunda !! Mungu ataendelea kunilinda na kunihifadhi, AmiinNisisahau kuwaambia, kadri mnavyoendelea kunizushia ndio jina la Governor De le boss linavyozidi kuwa kubwa”

“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments