Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Simba sasa bado kidogo tu!!! wapate nafasi ya kucheza na Everton

on

Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 umechezwa leo katika uwanja wa Afraha Nakuru nchini Kenya kwa kuzikutanisha timu za Simba SC na timu ya Kakamega Home Boys.

Game haikuwa nyepesi kama baadhi ya watu walivyokuwa wanatazamia, kiasi cha dakika 90 kumalizika ikiwa hakuna timu iliyokuwa imeona nyavu za mwenzake, mikwaju ya penati ndio iliamua mshindi w amchezo huo.

Simba Sports kwa mara ya pili mfululizo wanafanikiwa kuingia hatua inayofuata ya michuano hii kwa ushindi wa penati 5-4, ushindi huo sasa unaifanya Simba kuingia fainali huku wakisubiri mshindi kati ya Singida United na Gor Mahia ili kucheza nae fainali.

Kama Simba SC watafanikiwa kutwaa taji hilo la SportPesa Super Cup watafanikiwa kukata tiketi ya kucheza mchezo wa kirafiki na club ya Everton nchini England katika uwanja wa Godson Park uliyopo jiji la Liverpool.

AyoTV ilivyomnasa staa wa zamani wa Liverpool Airport KIA

Soma na hizi

Tupia Comments