AyoTV

KUTOKA JOHANNESBURG: Taifa Stars msikilizeni pia mwalimu Kashasha

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jumapili ya Novemba 18 2018 itakuwa Maseru Lesotho kucheza mchezo wake wa tano wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2019 nchini Cameroon, Taifa Stars game ya kwanza uwanja wa Chamazi ilitoka sare na Lesotho ya kufungana goli 1-1.

Mchezo wa marudiano ni muhimu zaidi kwa Taifa Stars iliyopo nafasi ya pili kwani ikiifunga Lesotho na Uganda wanaocheza Novemba 17 katika uwanja wao wa Namboole dhidi ya Cape Verde wakifanikiwa kupata ushindi basi Tanzania itakuwa imefuzu kucheza AFCON 2019 nchini Cameroon.

Kuelekea mchezo huo ambao kuna mashabiki wa Taifa Stars wametoka Tanzania na kwenda Lesotho kuisapoti Taifa Stars wakiungana na watanzania waishio Afrika Kusini, kuelekea mchezo huo AyoTV ikiwa Johannesburg Afrika Kusini imefanya exclusive na mchambuzi wa soka mwali Kashasha ambaye ameeleza mawazo yake kuhusiana ni kipi Taifa Stars wafanye.

Watanzania waishio Afrika Kusini wamejipanga kuelekea Lesotho leo

Shangwe zimeanzia Johannesburg hata kabla ya kufika Lesotho

Soma na hizi

Tupia Comments