PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Serie C wamejitutumua hadi 16 bora ya Coppa Italia

on

Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Coppa Italia ni timu mbili ndio zinatoka Serie C huku zikikutana na vilabu kutoka jijini Roma, Novara watakaocheza dhidi ya Lazio huku Virtus Entella wakicheza dhidi ya AS Roma siku ya Jumatatu.

Timu nyingine ambayo haitokei Serie A ni Benevento ambao watasafiri kuelekea Milan ambako watacheza dhidi ya Inter, huku ikitarajiwa kwamba vilabu vingi vikubwa vitashinda, mechi kati ya Bologna na Juventus itakuwa kivutio zaidi.

Juventus tayari wako kileleni mwa Serie A wakiwa point 9 mbele ya Napoli ambao wako nafasi ya pili, club hiyo ya jijini Turin itataka kujihakikishia ushindi dhidi ya Bologna ambao ni wa tatu kutoka mwisho katika msimamo wa Serie A, ili wawe katika nafasi nzuri ya kushinda kombe hilo kwa mara ya 14.

Kikosi cha Massimilano Allegri bado hakijapoteza mchezo wowote katika ligi za ndani kwa msimu huu, huku kikosi chao kikiwa na utajiri hasa eneo la ushambuliaji wachezaji kama Cristiano Ronaldo, Paulo Dybala na Mario Mandzukic, itakuwa jambo la kushangaza endapo watapoteza mchezo huo licha ya kuwa ugenini.

Ronaldo amefunga jumla ya magoli 14 katika ligi, goli moja pungufu ya magoli ambayo kikosi kizima cha Bologna kimefunga (15), mreno huyo amekuwa katika kiwango kizuri tangu alipowakacha mabingwa wa Ulaya Real Madrid game hizo zinataoneshwa na StarTimes pekee.

Mpenja katangaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake

Soma na hizi

Tupia Comments