Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA 4: Thomas Ulimwengu amesaini Sudan

on

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars aliyewahi kuvichezea vilabu vya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na club ya AFC Eskilstuna ya Sweden Thomas Ulimwengu baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu leo amepata timu.

Thomas Ulimwengu alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jereha lake la goti na baada ya kupona alijiunga na AFC Eskilstuna ya Sweden na kupata jeraha tena la goti liloendelea kumuweka nje ya uwanja tena kwa muda mrefu.

Leo Thomas Ulimwengu ameripotiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na club ya Al Hilal ya Sudan, hiyo inakuja ikiwa zimepita siku chache toka zimalizike tetesi za kuwa alitaka kusaini club ya nchini Bosnia.

VIDEO: Ukimuuliza John Bocco ana-miss nini Azam FC atakujibu hivi

Soma na hizi

Tupia Comments