Michezo

Mshambuliaji wa Bundesliga mwenye asili ya Tanzania kapewa mkataba mpya

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark anayeichezea club ya RB Leipzig ya Ujerumani Yusuf Poulsen club yake imetangaza kumuongezea mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kubakia Bundesliga, Poulsen kama hufahamu ndio yule staa wa Bundesliga mwenye asili ya Tanzania na Denmark.

Baada ya Poulsen kuongeza mkataba huo wa miaka mitatu za sasa ataendelea kubakia RB Leipzid katika 2022, Poulsen ambaye anaasili ya Tanzania upande wa baba yake akitokea Chumbageni Tanga, alikuwa sehemu ya kikosi cha Denmark kilichocheza fainali za Kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri baba yake mzazi Yussuf mzee Yurary alifariki kwa kansa wakati Yussuf akiwa na umri wa miaka 6, mama yake ni raia wa DenmarkYussuf Poulsen wengi tumemfahamu hivi karibuni baada ya mafanikio yake Bundesliga.

Poulsen akiwa na bibi yake na Girlfriend wake wakiwa Tanga

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke 

Soma na hizi

Tupia Comments