Biko


Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Kesho Kenya wanafunga usajili, Yanga vipi wameamuaje kuhusu Haji Mwinyi

on

Dirisha la usajili nchini Kenya linaripotiwa kuwa litafungwa kesho December 30 lakini awali tulisikia beki wa pembeni wa Yanga Haji Mwinyi kutakiwa na club ya AFC Leopards ya Kenya na tulisikia beki huyo akiomba Yanga imuachie aondoke kutokana na kukosa namba Yanga.

Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa ameongea na waandishi wa habari leo na kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo suala la Haji Mwinyi ambaye tayari amejumuika na wenzake katika kikosi kitakachocheza dhidi ya Mbao FC weekend hii jijini Mwanza.

“Ni kweli tulipata taarifa na nilipigiwa simu na viongozi wa AFC Leopards lakini nikawaambia kiutaratibu inabidi mtuletee barua kama mnamtaka mchezaji ili tuweze kuzungumza na mchezaji mwenyewe na kufuata taratibu ila hadi sasa sijapata hiyo barua”>>> Boniface Mkwasa

“Nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba”-Haji Manara

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement