PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

AyoTV

AyoTV ilivyomnasa staa wa zamani wa Liverpool Airport KIA

on

Baada ya mwaka 2017 Tanzania kutembelewa na mastaa mbalimbali wa soka kutoka Barani Ulaya na kuja Tanzania kutalii, leo usiku wa June 1 kuamkia June 2 beki wa zamani wa club ya Liverpool Martin Skrtel amewasili Tanzania akiwa na familia yake kwa mara ya kwanza.

Mke na mtoto wake

Kama hufahamu Martin Skrtel pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Czechoslovakia na amecheza club ya Liverpool kwa miaka nane jumla ya game 242 kuanzia mwaka 2008 hadi 2016 alipoamua kujiunga na club ya Fenerbahce ya Uturuki ambayo anaichezea hadi sasa.

Martin Skrtel

Martin Skrtel sio staa wa kwanza wa soka barani Ulaya kuwahi kuja Tanzania wakati wa likizo, bali wamewahi kuja David Beckham na familia yake, Mamadou Sakho na familia yake na staa wa Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen.

VIDEO: Mazoezi binafsi ya Simon Msuva na mdogo wake wakati huu akiwa likizo

Soma na hizi

Tupia Comments