Michezo

Simba SC kazi kwao kuupanda mlima, Yanga ndio hao

on

Club ya Dar es Salaam Young Africans leo imeendeleza jitihada zake za kuhakikisha wanaurejesha Ubingwa wao wa Ligi Kuu mikononi mwao, baada ya msimu uliopita kuupoteza na kuchukuliwa na wapinzani wao wa jadi Simba SC.

Yanga wameonesha dhamira hiyo kutokana na kuhakikisha wanapata matokeo chanya kwa kila mchezo, hivyo mchezo wa leo wa Yanga dhidi ya JKT Tanzania uwanja Taifa DSM, umethibitisha jitihada za Yanga kutaka kurudisha taji hilo kwa kupata ushindi wa magoli 3-0.

Magoli ya Yanga yalitiwa nyavuni na Mcongomani Heritier Makambo dakika ya 20, Mrisho Ngassa dakika ya 53 na goli la mwisho likafungwa na Ibrahim Ajib kwa mkwaju wa penati dakika ya 79 kufuatia mchezaji wa JKT Tanzania kuushika mpira uliopigwa na Thabani Kamusoko ndani ya eneo la 18.

Yanga sasa inaipa mtihani Simba SC kuweza kuifikia kwani hadi sasa Yanga inaizidi Simba SC point nane na mchezo mmoja, hivyo Simba wana mlima mrefu wa kupanda ili waifikie Yanga iliyopo nafasi ya kwanza kwa kuwa na point 35 wakicheza michezo 13, Simba nafasi ya tatu kwa point 27 tofauti ya point sita na Azam FC waliopo nafasi ya pili kwa kuwa na point 33.

EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?

Soma na hizi

Tupia Comments