Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Derby County hawana tatizo na Lampard, watoa sharti hili kwa Chelsea

on

Baada ya kubahinika kuwa club ya Chelsea ya England haina mpango tena na kocha Maurizio Sarri, habari zinazoripotiwa sasa ni kuhusu upatikanaji wa mbadala wa Maurizio Sarri zina ukweli, kuna dalili kuwa Frank Lampard ambaye ni kocha wa club ya Derby County inayoshiriki Championship ndio atakuwa mbadala wa Maurizio Sarri.

Kwa upande wa club anayoifundisha Frank Lampard imedaiwa kuwa licha ya kuwa na mkataba na staa huyo lakini wamemruhusu kujiunga na Chelsea kama atapenda ila kwa sharti la Chelsea kuilipa Derby County fidia ya pound milioni 4 ili kuvunja mkataba na kumalizana vizuri.

Chelsea ambayo imekuwa na hulka ya kubadilisha makocha mara kwa mara kwa kipindi kifupi, inataka kuanza kufundishwa na mchezaji aliyekulia katika timu yao, Frank Lampard anayehusishwa kurudi Chelsea kama  kocha wao, Lampard amewahi kuichezea Chelsea kwa miaka 13 toka alipojiunga nayo 2001 akitokea West Ham United baada ya kuwa kwa mkopo Swansea ila aliondoka Chelsea 2014 na kujiunga na Man City halafu New York City.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments