Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Wakazi Mloganzila walivyosimama barabarani kuzuia msafara wa RC Makonda

on

November 26 2016 ziara ya Dar Mpya ilikuwa Ubungo ambapo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alitembelea kampasi ya chuo na hospitali ya taaluma na tiba ya chuo kikuu cha afya na sayanzi shirikishi, Muhimbili iliyoko Mloganzila, wakati akiondoka  eneo hilo wananchi walisimama barabarani kuzuia msafara wakidai kutopewa fidia baada ya nyumba zao kubomolewa kupisha mradi huo.

Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole aliwaambia wananchi hao kuwa suala lao linashughulikiwa na wengi wao ameshaonana nao akawambia wakalete taarifa za ziada ili awatafutie msaada wa kisheria ila hawakurudi hivyo DC polepole akawaomba wafuate utaratibu.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alisimama na kuwaambia ni marufuku kwa yeyote kuzuia msafara kwa kuwa hakuna kero itakayotatuliwa kwa kuzuia msafara hivyo wafuate walichoambiwa na Mkuu wa wilaya. Unaweza kuangalia video hii hapa chini.

VIDEO: Alichokiongea RC Makonda baada ya kutembelea MUHAS Kampasi ya Mloganzila 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement