PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Arusha United ndio hawa, wanaitaka Ligi Kuu TZ 2019/20

on

Club ya Arusha United leo Jumamosi ya September 29 2018 inaanza rasmi harakati za kuipambania nafasi ya kucheza Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2019/20, kwani iko Karatu kwa kambi maandalizi ya mchezo wao wa leo.

Arusha United leo inaanza safari ya game yake ya Ligi Daraja la kwanza dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora, game hiyo itachezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kama ufahamu Arusha United inatabiriwa kuwa itapanda Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2019/20 kutokana na wachezaji walionao na kocha waliyenae Fred Felix Minziro ambaye amepandisha Ligi Kuu Vilabu kama Singida United na KMC ya Kinondoni.

JB na Ray “Hata Yanga wao wanajua Simba ana timu bora”

Soma na hizi

Tupia Comments