Michezo

VIDEO: Samatta baada ya kuwa kinara wa magoli Ubelgiji

on

Usiku wa October 31 2018 Mbwana Samatta na timu yake ya KRC Genk walicheza game yao ya Ligi Kuu Ubelgiji ugenini dhidi ya Antwerp, mchezo huo ulimalizika kwa Genk kupata ushindi wa magoli 4-2, Samatta akifunga magoli mawili kati ya hayo.

Samatta baada ya kufunga magoli mawili anafikisha jumla ya magoli 10 na kuongoza msimamo wa wafungaji Ligi Kuu Ubelgiji, Genk ikiongoza Ligi kwa kuwa na jumla ya point 33 ikifuatiwa na Club Brugge iliyopo nafasi ya pili kwa kuwa na point 30.

Baada ya Samatta kufunga magoli hayo alifanyiwa interview na Genk TV na kufunguka “Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwetu kila mmoja aliona nafikiri ni kutokana na kucheza mechi mfululizo kila baada ya siku tatu lakini najivunia timu yangu kwa sababu tulikuwa imara”

“Nafuraha kwa sababu nimefikisha magoli 10 katika Ligi lakini najivunia zaidi kuwa vinara wa Ligi, kwangu ni bora zaidi kufanikiwa kama timu kuliko mimi kuongoza ufungaji bora, nimekuwa nikifanya mazoezi sana sio rahisi kufunga magoli”

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments