Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Emmanuel Okwi hawezi kupata presha kwa rekodi ya Tambwe VPL

on

Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea leo Jumapili ya May 6 2018 wekundu wa Msimbazi Simba walikuwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuikaribisha Ndanda FC kucheza mchezo wao wa 27 wa Ligi Kuu msimu wa 2017/2018.

Katika mchezo huo Simba walipata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 44 ya mchezo, goli hilo limemfanya Emmanuel Okwi kufikisha jumla ya magoli 20 ya VPL msimu huu akibakisha magoli mawili avunje rekodi ya Amissi Tambwe aliyokuwa kawa mfungaji bora wa VPL kwa kufunga magoli mengi (21) kwa msimu mmoja.

Baada ya game AyoTV iliongea na Emmanuel Okwi “Nashukuru Mungu nimeweza kucheza vizuri mpaka sasa nimefunga magoli hayo lakini mimi rekodi za watu haziwezi kuniweka katika presha ninachoangalia kuisaidia timu yangu kupata ushindi”

VIDEO: Mbwembwe za Haji Manara uwanjani baada ya ushindi wa Simba vs Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments