Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Takwimu za Abdi Banda Afrika Kusini baada ya leo kufunga magoli mawili PSL

on

Beki wa kati wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya Baroka FC ya Afrika Kusini Abdi Banda leo amerudi tena kwenye headlines baada ya kuifungia timu yake katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu Afrika Kusini msimu wa 2017/2018 dhidi ya Bloemfontein Celtic.

Abdi Banda ambaye kwa sasa ni moja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha Baroka FC amezidi kuonesha uwezo kiasi cha kufikia kuisadia timu yake kufunga magoli katika game dhidi ya Bloemfontein Celtic, leo Baroka ilikuwa nyumbani kucheza mchezo wake wa 29 wa Ligi Kuu Afrika dhidi ya Bloemfontein Celtic na kulazimishwa kutoka sare ya 2-2.

Baroka FC ndio walikuwa wa kwanza kuruhusu goli dakika ya 60 baada ya mchezaji Sepana Letsoalo wa Bloemfontein Celtic kufunga goli la uongozi, baada ya hapo Baroka FC wakachomoa na kufunga goli la kwanza na pili kupitia kwa Abdi Banda dakika ya 62 na 80 lakini hawakufanikiwa kuzibakisha point zote tatu nyumbani baada ya dakika ya 90 Kabelo Dlamini akaisazishia goli Bloemfontein Celtic ya safu ya ulinzi ya Baroka kujisahau.

Sare hiyo sasa inaifanya Baroka kuwa nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu Afrika Kusini unaoshirikisha jumla ya timu 16, wakiwa na point 34 lakini kwa upande wa Banda baada ya kufunga leo anakuwa ameifungia Baroka magoli matatu baada ya kufunga goli lake la kwanza dhidi ya Orlando Pirates na sasa bado game mmoja Ligi yao imalizike.

Hata hivyo kama hufahamu Banda amekiwa na wakati mzuri na Baroka FC kutokana na kufanikiwa kucheza jumla ya mechi 31, 27 za Ligi na nne za mashindano mengine na kati ya game 31 alizocheza ni mechi moja pekee dhidi ya Free State February 3 2018 ndio alicheza kwa dakika 63 ila game nyingine zote alicheza kwa dakika zote 90, hadi sasa ameoneshwa jumla ya kadi tatu za njano.

VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao

Soma na hizi

Tupia Comments