Michezo

PICHA 4: Mchezaji Henry Joseph afunga ndoa

on

Kiungo wa zamani wa club ya Simba SC anayecheza soka katika club ya Mtibwa Sugar ya Morogoro Henry Joseph Shindika amefanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Oliver.

Henry ambaye aliwahi kuwa nahodha wa Taifa Stars amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu November 9 2018 katika jiji la Mwanza huko ndio anakotokea Henry Joseph.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Henry Joseph amewahi kucheza Simba SC 2006-2008 baadae akajiunga na Club ya Kongsvinger ya Norway aliyodumu nayo miaka minne kabla ya kurejea Simba SC tena 2013-2014 akaenda Mtibwa Sugar hadi sasa.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments