AyoTV

Simba SC wapo moto Haruna Niyonzima kawaweka Mlandege FC

on

Wekundu wa Msimbazi Simba Jumatano ya January 9 watarejea Dar es Salaam kwa ajili ya Maandalizi ya mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi wa michuano ya CAF Champions League dhidi ya JS Saouro ila kabla ya kwenda usiku wa January 8 ilicheza game yake ya mwisho ya Makundi ya Mapinduzi Cup dhidi ya Mlandege.

Simba SC wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mlandege goli ambalo limefungwa na Haruna Niyonzima dakika ya 21 ya mchezo kwa penati, hivyo Simba imemaliza game zake za Kundi B ikiwa imepata ushindi katika michezo yao yote mitatu na kuvuna jumla ya point 9.

Baada ya kuwa kinara wa Kundi B Simba watacheza game ya nusu fainali dhidi ya timu iliyomaliza nafasi ya pili Kundi A, ambapo Simba sasa kwa michezo iliyobakia italeta Team B imalizie michuano hiyo kwani haitaweza kurudi Zanzibar kutokana na ratiba kubana.

Mpenja katangaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake

Soma na hizi

Tupia Comments