Michezo

Hazard anataka kwenda Real Madridi kwa style ya Ronaldo

on

Moja kati ya majina makubwa yanayotajwa katika usajili wa dirisha dogo la mwezi January ni pamoja na kiungo wa Chelsea raia wa Ubelgiji Eden Hazard anayehusishwa kwa karibu kujiunga na  club ya Real Madrid ya Hispania, kuna uwezekano mkubwa hilo likatokea kutokana na kauli yake aliyoitoa.

Hazard ameeleza kuwa ana hamu ya kwenda kucheza Real Madrid kwa siku za usoni licha ya kuwa ameripotiwa kuwa katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Chelsea.

“Kwa sasa sitaki kusema nitasaini mkataba mpya halafu mwisho wa siku nisisaini, hivyo nitaangalia maana kuna wakati naamka nasema nataka kuondoka na kuna wakati naamka nasema nataka kubaki”>>>Hazard

Kauli ya Hazard ya kuanza kuonesha kuwa bado hajafanya maamuzi ya moja kwa moja inahusishwa na staa wa zamani wa Man United Cristiano Ronaldo ambaye aliondoka Man United dakika za mwishoni  na kujiunga na Real Madrid wakati alikuwa akionesha dalili za kutaka kuendelea kuitumikia club hiyo 2009.

Samatta alivyofutwa miguu baada ya game

Soma na hizi

Tupia Comments