Michezo

Baada ya kugoma kucheza, Adebayor kaitwa tena pale pale

on

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Togo Claude LeRoy raia wa Ufaransa ameamua kumuita Emmanuel Adebayor kwenye kikosi cha wachezaji 23, watakaocheza game ya kuwania kufuzu kucheza mataifa ya Afrika 2019 (AFCON 2019) Cameroon.

Claude LeRoy pamoja na Adebayor kukataa kucheza mchezo wa kuwania kufuzu kucheza mataifa ya Afrika dhidi ya Gambia kwa madai ya kutoridhishwa na uwanja wa nyasi bandia katika mji wa Lome kitu kilichopelekea kuukosa pia mchezo wa marudiano nchini Gambia.

Wengi walitafsiri kuwa kitendo cha Adebayor kugoma kucheza game hiyo iliyomalizika kwa kufungana goli 1-1 na mchezo wa marudiano ugenini kushinda 1-0, kitendo cha Adebayor ni kinatafsiriwa kama utovu wa nidhamu, hivyo kuna uwezekano kuwa angekosa kuitwa tena na kocha huyo raia wa Ufaransa kama sehemu ya kumuadhibu.

LeRoy kabla ya kutangaza kikosi alithibitisha kufanya mazungumzo na Adebayor na amemthibitishia kuwa atacheza game dhidi ya Algeria, kwenye uwanja huo huo aliokataa kucheza mwezi October Lome nchini Togo, kwa sasa Tongo wapo nafasi ya katika Kundi lao D lenye timu za Algeria, Gambia na Benin.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments