Top Stories

Pilau lasababisha jamaa kuangua kilio harusini

on

Leo Juni 20, 2018 nakusogezea stori kutoka nchini Kenya ambapo unaambiwa kuwa Jamaa mmoja amegeuka kituko baada ya kuangua kilio alipoambiwa kuwa pilau limeisha kwenye harusi aliyohudhuria.

Imeelezwa kuwa Jamaa huyo ambaye alifika katika harusi hiyo kwa kuchelewa alienda moja kwa moja mpaka kwa Wapishi akiwataka wampe pilau na ndipo alipoambiwa kuwa pilau limeisha na kuanza kuangua kilio kizito.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa baada ya jamaa huyo kuambiwa hivyo alianza kutokwa na machozi.

“Jamaa alibaki tu amesimama huku akiyaangalia masufuria huku akitokwa na machozi”,alisema shuhuda huyo ambaye hakutaka kujulikana.

Taarifa zinaendelea kusema kuwa wageni wengine waliokuwa wamehudhuria katika harusi hiyo walibaki kumuangalia jamaa huyo huku wengine wakimuonea huruma na wengine wakikisia kuwa huenda Jamaa huyo hakuwa na chakula nyumbani kwake.

Hata hivyo baadhi ya vijana waliohudhuria harusi hiyo iliwabidi wamfukuze Jamaa huyo wakidai kuwa anatia aibu harusini.

Lema kawafungukia wanaosema kafulia na gari yake ya mwaka 1962

Soma na hizi

Tupia Comments