Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Sanchez amehukumiwa miezi 16 jela

on

Leo February 9, 2018 nakusogezea stori kutoka kwa Staa mpya wa klabu  ya Manchester United Alexis Sanchez amehukumiwa jela miezi 16 kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi.

Hukumu hiyo imetolewa February 8, 2018 , Sanchez anadaiwa kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa nchini Uhispania ambapo mamlaka nchini humo zinasema anadaiwa kiasi cha pauni laki tisa.

Kwa mujibu wa sheria za Hispania, hukumu ya kosa hilo haizidi miaka miwili jela, lakini badala yake amelipa pauni 525,000 kutokana na kosa ambalo alilifanya miaka mitatu alipokuwa akichezea klabu ya Barcelona.

Hukumu ya Sanchez imekuja katika kipindi ambacho bado mamlaka za mapato nchini Hispania zinafanya uchunguzi kuhusu kocha Jose Mourinho anaye tajwa kufanya kosa kama hilo.

MANARA AMEWAOMBA MASHABIKI WA SIMBA WAKAISHANGILIE YANGA

HAMISA MOBETTO KAFUNGUKA MAHAKAMA KUMSULUHISHA NA DIAMOND “UGOMVI WA FAMILIA UACHENI TU”, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments